Isaiah 66:15-16


15 aTazama, Bwana anakuja na moto,
magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,
atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,
na karipio lake pamoja na miali ya moto.

16 bKwa maana kwa moto na kwa upanga wake
Bwana atatekeleza hukumu juu ya watu wote,
nao wengi watakuwa ni wale
waliouawa na Bwana.

Copyright information for SwhKC